Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bonde la Wami Ruvu

Bonde le wami Ruvu linajumuisha mito mikuu miwili ambayo ni Wami wenye kilometa za mraba 400000 na Ruvu kilometa za mraba 17700. Pamoja na mito ya ukanda wa Pwani iliyopo Kusini mwa Dar es salaam. Bonde hili kwa ujumla linaukubwa km za mraba 72930 pia lina maeneo ya tambarare na safu ndefu za milima. 
Kuna aina nne za milima katika bonde hili ambazo ni:

  •  Milima ya Uluguru iliyopo Kusini Mashariki (altitude 400 mpaka 2500m)
  •  Milima ya Nguru iliyopo Magharibi ya Kilosa (altitude 400 mpaka 2000m)
  •  Milima ya Rubeho iliyopo Magharibi ya Kilosa (altitude 500 mpaka 1000m)
  •  Milima ya Ukaguru iliyopo Kaskazini mwa Wami (altitude 400 mpaka 1000m)