Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bonde la Mto Ruvuma

Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini lina mito mikuu mitano inayomwaga maji yake katika bahari ya Hindi. Mito hiyo ni Mto Matandu wenye kilometa za mraba 18,565, Mto Mavuji wenye kilometa za mraba 5,600, Mto Mbwemkuru wenye kilometa za mraba 16,255, Mto Lukuledi wenye kilometa za mraba 12950 na vijito vya mto Ruvuma.

Maeneo ya mabonde madogo yapo kati ya altitudi 305-710 juu ya usawa wa bahari, na hutiririsha maji yake kuelekea ukanda wa pwani. Mto Ruvuma unashirikiana kati ya Tanzania na Msumbiji na unamwaga maji yake katika bahari ya Hindi. Mto huu una urefu wa kilometa 800 kati ya hizo kilometa 650 zipo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Bonde la mto Ruvuma lina ukubwa wa kilometa za mraba 152,200 kati ya hizo kilometa 52,200 (34.3%) zipo Tanzania na kilometa 99,530 (65.39%) zipo Msumbiji na Malawi kilometa 470 (0.31%). Vijito vikubwa vya mto huu kwa upande wa Tanzania vimeanzia katika wilaya za Mbinga, Tunduru na Masasi. Wastani wa maji yanayoingia mto Ruvuma kwa mwaka ni mita za ujazo 15,000 milioni.
Bonde la mto Ruvuma na pwani ya kusini lina ukubwa wa kilomita za mraba 104,270 na idadi ya watu wapatao 2,241,944. Wastani wa nyuzi joto ni 260C kwa ukanda wa pwani na nchi kavu nyuzi joto 24, mabadiliko ya hali ya joto kwa siku na mwaka hutokea