Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bodi ya Maji ya Taifa

Bodi ya Maji ya Taifa (National Water Board)

Usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji nchini unaongozwa na Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2009. Sera inaelekeza kuwa rasilimali za maji zitasimamiwa katika ngazi zifuatazo:

  • Ngazi ya Taifa,
  • Ngazi ya Bonde,
  • Ngazi ya Bonde dogo (catchment/subcatchment),
  • Ngazi ya Wilaya,
  • Jumuiya za watumiaji maji.

Majukumu ya kila ngazi yameainishwa kwenye sheria ambayo pia imetoa mfumo wa kitaasisi na kisheria wa usimamizi na uendelezaji endelevu wa rasilimali za maji.

Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa